TyDiQA1.0

The Typologically Different Question Answering Dataset

Predictions

Scores

Wingu la Oort

The Typologically Different Question Answering Dataset

Wingu la Oort (ing. Oort cloud) ni ukanda wa kudhaniwa angani unaozunguka mfumo wa Jua kwa umbali mkubwa nje ya mzingo wa Pluto pia nje ya ukanda wa Kuiper. Ukanda huu unadhaniwa kuwa na magimba ya barafu na vumbi yaliyo na mwendo wa kuzunguka Jua kwa umbali kuanzia vizio astronomia 50,000 hadi 100,000 au zaidi (sawa na miaka ya nuru 0.8 hadi 1.5). Kuwepo kwa wingu hili hakuthibitishwa kwa hiyo ni bado wingu la kinadharia. Nadharia hii ilitungwa na mwanaastronomia Mholanzi Jan Oort (1900 – 1992) aliyetafuta maelezo kwa asili na njia za nyotamkia zinazotokea katika mfumo wa Jua. Wingu la Oort linatazamiwa kuwa asili ya nyotamkia zenye obiti ndefu, ilhali zile zenye obiti fupi zinatoka katika Ukanda wa Kuiper.[1]

Wingu la Oort liligunduliwa na nani?

  • Ground Truth Answers: Jan OortJan Oort

  • Prediction:

Jan Oort aliunda nadharia kuhusu wingu hili alipotafuta maelezo ya kuwepo kwa nyotamkia zenye obiti ndefu yaani zinazorudi baada ya miaka mingi. Kabla yake walikuwepo wengine waliowaza ya kwamba asili ya nyotamkia iko kwenye mipaka ya nje ya mfumo wa Jua. Oort aliwaza ya kwamba kuna magimba madogo mengi yanayozunguka Jua kwa umbali mkubwa. Kimsingi yapo katika obiti thabiti. Lakini mara kwa mara graviti ama ya nyota jirani -maana wingu linaenea hadi robo au nusu ya umbali kati ya Jua na nyota jirani ya Rijili Kantori (A Centauri)- na pia athari ya graviti ya sayari kubwa ndani ya mfumo wa Jua inaweza kuleta vurugu kwa obiti za magimba kadhaa na hivyo yanaanza kuvutwa na Jua na kuingia katika obiti itakayopita katika sehemu za ndani za mfumo wa Jua. Kama zinakaribia Jua zinapashwa moto, barafu ya miili yao inaanza kuyeyuka na "mkia" wa gesi inayoakisia nuru unaonekana.[3]

Wingu la Oort liligunduliwa na nani?

  • Ground Truth Answers: Jan Oort

  • Prediction: